"JE! WEWE UNGETHUBUTU KAMA MTOTO HUYU?

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids.com

Kulikua na mtoto mmoja alisikia habari kwamba kutafanyika mashindano ya kukimbia yatakayowashirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali. Habari hiyo iliwafurahisha wengi lakini baadhi ya watoto waliogopa kushiriki kwa kuhofia kushindwa.

Mtoto huyo alitamani sana kushiriki mashindano hayo ingawa hakuwahi kushindana hapo awali. Alijua kuwa ili afanikiwe alihitaji kufanya mazoezi kwa bidii. Kila siku baada ya masomo alitumia muda wake kufanya mazoezi ya kukimbia na kujitayarisha kwa mashindano.

Siku zilivyopita baadhi ya wenzake walimkatisha tamaa kwa kumwambia kuwa asingeshinda kwa sababu alikuwa mdogo na hana uzoefu. Badala ya kukata tamaa aliamua kuendelea kujituma na kuamini uwezo wake.

Hatimaye siku ya mashindano ilifika. Washiriki wengi walijitokeza na ushindani ulikuwa mkubwa. Mbio zilipoanza mtoto huyo hakuanza kwa kasi sana lakini aliendelea kukimbia kwa nguvu na uvumilivu. Kadiri mashindano yalivyoendelea aliwaacha washiriki wengi nyuma.

Mwisho wa mbio aliweza kufika mstari wa mwisho akiwa wa kwanza. Watu wote waliokuwapo walishangilia na kumpongeza kwa juhudi na ujasiri wake. Furaha ilitawala kila mahali kwa sababu alikuwa amethibitisha kuwa kuthubutu na kufanya kazi kwa bidii huleta mafanikio.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments