Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mwalimu ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto baada ya mzazi. Mara nyingi mwalimu huitwa mzazi wa pili kwa sababu anashiriki katika malezi na makuzi ya mtoto akiwa shuleni. Ingawa mzazi humlea mtoto nyumbani mwalimu naye ana jukumu la kumfundisha na kumkuza kiakili na kitabia.
Shuleni mwalimu humfundisha mtoto masomo mbalimbali kama vile hisabati, lugha, sayansi na mengine. Lakini si elimu tu mwalimu pia humfundisha mtoto maadili mema kama heshima, utii, ushirikiano na nidhamu. Haya yote humsaidia mtoto kuwa na tabia nzuri katika jamii.
Pia mwalimu humsaidia mtoto kutambua tofauti kati ya mema na mabaya. Anapomrekebisha mtoto anapofanya makosa humfundisha jinsi ya kuwa mtu bora katika maisha yake ya baadaye. Kwa njia hii mwalimu huchangia kwa kiasi kikubwa katika malezi ya mtoto.
Hata hivyo ni muhimu kuelewa kuwa mwalimu hawezi kuchukua nafasi kamili ya mzazi. Wazazi na walimu wanapaswa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha mtoto analelewa vizuri. Ushirikiano huu hujenga msingi imara wa mafanikio ya mtoto.
Mwalimu anaitwa mzazi wa pili kwa sababu ana mchango mkubwa katika kumlea na kumkuza mtoto. Kazi ya mwalimu ni ya thamani kubwa na inapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa na jamii nzima.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment