Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Ilikuwa Jumamosi jioni. Familia ya kina Rehema ilikuwa imekusanyika sebuleni. Baba alikuwa akiangalia habari kwenye televisheni, mama alikuwa akipika jikoni na Rehema pamoja na mdogo wake Musa walikuwa wakifanya kazi zao za shule.
Ghafla taa zikazimika. Televisheni ikanyamaza, feni zikasimama na nyumba ikawa giza.
"Umeme umekatika!" Musa alisema kwa sauti ya mshangao.
Mwanzoni watoto walihuzunika. Hawakuweza kuangalia televisheni wala kutumia simu za wazazi wao kucheza michezo.Mama akawasha mshumaa na kuuleta sebuleni. Mwanga wake mdogo uliangaza chumba. Baba akasema
"Badala ya kulalamika hebu tutumie muda huu kuzungumza pamoja."
Kila mmoja alianza kusimulia hadithi za kuvutia. Baba alisimulia jinsi alivyokuwa akienda shule kwa miguu kilomita kadhaa alipokuwa mtoto. Mama naye alisimulia mchezo waliokuwa wakicheza kijijini wakati wa mwezi.
Rehema na Musa walifurahia sana kusikiliza hadithi hizo. Baadaye walicheza mchezo wa kutegana vitendawili na wote wakacheka kwa furaha.
Muda ulipita haraka bila wao kutambua. Ghafla taa zikarudi. "Umeme umerudi!" Musa alipaza sauti.Lakini safari hii hakuna aliyekimbilia televisheni. Walikuwa bado wanafurahia mazungumzo yao.
Rehema akasema "Leo nimejifunza kwamba tunaweza kufurahi hata bila umeme." Wazazi wake walitabasamu kwa furaha.
emakulatemsafiri@gmail
0653903872



Post a Comment