Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Kulikuwa na msichana mmoja aliyeishi na wazazi wake.Alikuwa na tabia nzuri na alipenda sana kusoma vitabu pamoja na kucheza na marafiki zake baada ya kutoka shule.
Siku moja akiwa darasani alianza kuhisi maumivu tumboni na mwili wake ulikuwa mzito kuliko kawaida. Alijaribu kuvumilia hadi muda wa mapumziko ulipofika. Alipoenda chooni alishtuka kuona damu kwenye nguo yake.
Aliingiwa na hofu kubwa kwa sababu hakuelewa kilichokuwa kinaendelea. Alibaki kimya hadi aliporudi nyumbani jioni hiyo.
Mama yake alipomuona akiwa mtulivu sana kuliko kawaida alimkaribia na kumuuliza kulikuwa na nini. Kwa aibu na wasiwasi alimweleza kuhusu damu aliyokuwa ameiona shuleni.
Mama yake alimshika mkono na kumwambia kwa upole “Usiogope mwanangu. Hiyo ni hedhi ni jambo la kawaida kwa msichana anayekua.”
Mama alimfundisha jinsi ya kutumia pedi, umuhimu wa usafi wakati wa hedhi na namna ya kujitunza vizuri. Pia alimweleza kuwa hedhi si jambo la kuogopa wala la kuaibika.
Alimsikiliza mama yake kwa makini na akaanza kuelewa mabadiliko yaliyokuwa yanatokea mwilini mwake. Siku hiyo alijisikia mwenye amani zaidi na akaendelea na maisha yake akiwa na uelewa mpya kuhusu ukuaji wa msichana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment