Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale kulikuwa na kijana mdogo aitwaye Kito aliyeishi kijijini karibu na msitu mkubwa. Kito alipenda sana kusaidia watu na kucheza na wanyama.
Siku moja alipokuwa akikusanya kuni alisikia sauti ndogo ikilia. Alifuata sauti hiyo mpaka akamwona sungura mdogo amenasa kwenye mtego. Kito alimhurumia sana akaufungua mtego na kumwachia.
Sungura alisema “Asante rafiki yangu wema wako hautapotea.”
Kito alishangaa kusikia sungura anaongea lakini alifurahi na kurudi nyumbani.
Baada ya siku chache kijiji kilipatwa na ukame mkubwa. Maji yakawa haba sana. Watu wote walihangaika kutafuta maji. Kito akaenda msituni kutafuta chemchemi.
Akiwa njiani yule sungura alitokea tena na kusema
“Nifuate". Sungura alimpeleka Kito kwenye chemchemi safi iliyokuwa imefichwa katikati ya mawe makubwa. Kito akakimbia kijijini kuwaambia watu. Wote walifurahi sana na kupata maji ya kutosha.
Mzee wa kijiji alisema “Wema wa Kito umeokoa kijiji chetu.”
Tangu siku hiyo watoto wote wa kijiji walijifunza kuwa kufanya wema huleta baraka.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment