Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto mmoja darasani kwetu. Hakuwa mtu wa kuongea sana wala hakujichanganya na wengine. Kila muda alikuwa kimya mara nyingi akiwa na vitabu vyake.
Kwa upande wangu sikuwahi kumchukulia seriously. Niliona kama hana ujasiri ukweli ni kwamba hata nilikuwa namdharau kidogo ndani kwa ndani. Sikuwa peke yangu wanafunzi wengi walikuwa wanamuona hivyo hivyo.
Sisi tulikuwa kundi la watu “maarufu” darasani. Tulipenda kelele, utani na kujiachia. Tuliamini sisi ndio tunaelewa maisha kuliko wengine.
Yeye? Alikuwa tofauti kabisa.
Muda ulivyoenda mtihani wa muhula ukakaribia. Wengine walikuwa wanaanza kujisomea lakini sisi tulikuwa bado kwenye michezo na stori.
Tuliamini tutafaulu tu bila hata jitihada kubwa.
Siku ya matokeo ilipofika hali ilikuwa tofauti kabisa na tulivyotarajia.
Majina yakaanza kutangazwa…
Nafasi ya kwanza yule yule mtoto tuliyekuwa tunamdharau.
Darasa zima likanyamaza.
Nilihisi aibu sana. Sio kwa sababu yeye amefaulu bali kwa sababu nilikuwa nimemhukumu bila kumjua.
Tangu siku hiyo nilianza kubadilika. Niligundua kuwa mtu haoneshi thamani yake kwa kelele au kujionesha.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment