Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Kila siku nilikuwa naanza asubuhi na simu mkononi.
Nilikuwa napitia mitandao picha, video na maisha ya watu wengine.
Kila mtu alionekana kuwa na maisha mazuri zaidi kuliko mimi.
Mavazi mazuri, simu mpya, safari na furaha…
Polepole nilianza kujilinganisha nao.Nilianza kuona kama maisha yangu hayatoshi. Nilihisi kama nimechelewa kufikia mafanikio fulani.
Hata vitu nilivyokuwa navyo havikunifurahisha tena.
Nilianza kuwa na mawazo mengi kujiona mdogo na kujiona sifai.
Hakuna mtu aliyenilazimisha kufikiria hivyo lakini nilikuwa najiumiza mwenyewe.
Siku moja nilikaa peke yangu nikitafakari.
Nilijiuliza “Je! ninajua maisha yao yote au ninaona sehemu tu?”
Ndipo nilipoanza kuelewa.
Watu wengi wanaonesha upande mzuri tu wa maisha yao. Hawaposti shida zao, hofu zao au changamoto wanazopitia.
Nilikuwa najilinganisha na picha iliyochaguliwa sio maisha halisi.
Kuanzia hapo nilianza kubadilika.
Nilipunguza muda wa mitandao. Nikaanza kuangalia maisha yangu mwenyewe kile nilichonacho na kile ninachoweza kufanya.
Polepole, amani ilirudi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment