Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Watoto hupenda ndoto na matumaini. Kila mtoto ana kipaji chake ambacho kinaweza kuleta mafanikio makubwa baadaye. Wapo wanaopenda kusoma, kucheza mpira, kuimba, kuchora au kufanya mambo ya ubunifu. Ni muhimu wazazi na walimu kutambua vipaji hivyo na kuwasaidia watoto kuviendeleza ili waweze kutimiza ndoto zao.
Pia watoto wanahitaji kuishi katika mazingira yenye amani na usalama. Vitendo vya ukatili matusi au unyanyasaji vinaweza kuwaumiza na kuathiri maisha yao. Jamii inapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata haki zao na kulindwa wakati wote. Serikali pamoja na mashirika mbalimbali yana jukumu la kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, huduma za afya na malezi yanayofaa.
Zaidi ya hayo watoto wanahitaji muda wa kucheza na kushirikiana na wenzao. Michezo huwasaidia kujifunza ushirikiano, uvumilivu na kujiamini. Wakati wa kucheza pia huwafanya wawe na furaha na afya nzuri ya mwili pamoja na akili. Familia zinazowapa watoto muda wa kuzungumza na kucheza nao hujenga mahusiano mazuri na yenye upendo.
Kwa ujumla mtoto ni tumaini la familia na taifa kwa ujumla. Tukiwalea watoto kwa upendo, maadili mema na elimu bora tutakuwa tunajenga jamii yenye watu wenye heshima, maarifa na mafanikio katika siku zijazo.
Emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment