Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Wakati wa mapumziko shuleni watoto walikuwa wakinunua chakula kwenye kibanda cha shule. Kila siku kulikuwa na msongamano mkubwa kwa sababu baadhi ya watoto walitaka kuhudumiwa haraka kuliko wengine.
Siku moja watoto wawili walianza kusukumana ili wafike mbele ya foleni. Chakula kikadondoka chini na wengine wakakosa nafasi ya kununua kwa muda ule.
Mwalimu aliyekuwa karibu aliwaita na kuwauliza: “Kwa nini hamfuati utaratibu wa foleni?”
Watoto walinyamaza kwa aibu.
Mwalimu akaamua kuwafundisha umuhimu wa kusubiri zamu yao. Kuanzia siku hiyo watoto wote walipanga mstari vizuri. Huduma ikawa ya haraka zaidi na hakukuwa tena na ugomvi.
Baada ya muda hata walipokuwa nje ya shule walianza kuheshimu foleni kwenye magari, dukani na hospitalini.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment