WATOTO NA MAADILI MEMA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Maadili mema ni msingi muhimu katika kumlea mtoto na kumjenga kuwa mtu mwema katika jamii. Watoto wanaofundishwa maadili mema tangu wakiwa wadogo hukua wakiwa na tabia nzuri na heshima kwa wengine.

Kwanza wazazi na walezi wana jukumu la kuwafundisha watoto maadili kama heshima, utii na upendo. Mtoto anapofundishwa kusema tafadhali na asante hujenga tabia ya kuthamini wengine.

Pili watoto wanapaswa kufundishwa kusema ukweli wakati wote. Uaminifu ni sifa muhimu ambayo humfanya mtu kuaminika katika jamii. Mtoto akizoea kusema uongo inaweza kuwa vigumu kubadilika baadaye.

Pia kuwahimiza watoto kusaidiana na wenzao ni sehemu ya maadili mema. Watoto wanapaswa kujifunza kushirikiana, kusaidia wenye uhitaji na kuepuka tabia mbaya kama wivu na chuki.

Aidha wazazi wanapaswa kuwa mfano mzuri kwa watoto wao. Watoto hujifunza zaidi kwa kuona kuliko kusikia hivyo wazazi wanapaswa kuonesha maadili mema katika matendo yao ya kila siku.

Hata hivyo changamoto kama ushawishi mbaya kutoka kwa marafiki, mitandao ya kijamii na ukosefu wa uangalizi zinaweza kuathiri maadili ya watoto. Ni muhimu kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwaongoza vizuri.

Kwa kumalizia maadili mema ni msingi wa maisha bora ya mtoto na maendeleo ya jamii. Tukiwafundisha watoto maadili mema leo tutakuwa na jamii yenye amani na mshikamano kesho.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments