Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Baraka alikuwa kijana aliyeishi na baba yake katika kijiji kidogo. Tangu akiwa mdogo alipenda sana magari. Kila alipoyaona yakipita macho yake yalikuwa yanang’aa.
Alikuwa akisema mara kwa mara: “Siku moja nitakuwa fundi mkubwa wa magari.”
Lakini watu wengi kijijini walimcheka: “Hiyo kazi ni ngumu sana… wewe huwezi!”
Licha ya maneno hayo Baraka hakukata tamaa. Baada ya kumaliza shule alianza kujifunza kazi ya ufundi kwenye gereji ndogo karibu na kwao. Mwanzoni alikuwa anafanya kazi ndogo ndogo ya kusafisha vifaa, kuosha magari na kusaidia mafundi wakubwa.
Miaka ilipita polepole akajifunza kila kitu kuhusu magari.
Siku moja gari la mteja liliharibika vibaya sana na mafundi wengine walishindwa kulitengeneza. Baraka aliomba ajaribu. Kwa umakini mkubwa alichunguza tatizo na hatimaye akalirekebisha!
Mteja alifurahi sana na habari zikaenea haraka.
Baada ya muda Baraka alifungua gereji yake mwenyewe na watu wengi walikuwa wanampeleka magari yao kwake.Wale waliokuwa wanamcheka zamani walikuja kusema: “Umefanikiwa kweli!”
Baraka alitabasamu na kusema “Ndoto yangu ilinifikisha hapa.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment