Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.
Kulikuwa na kijana mdogo aitwaye Omari aliyeishi na bibi yake katika kijiji cha Tulivu. Omari alikuwa na tabia moja mbayaalipenda sana kuahirisha mambo.Kila siku bibi yake alimwambia “Omari fanya kazi zako mapema.” Lakini yeye alikuwa akijibu “Nitafanya baadaye…”
Siku moja alipokuwa akisafisha chumba cha zamani cha bibi yake alikuta saa ya ajabu iliyokuwa imefunikwa na vumbi. Ilikuwa tofauti na saa nyingine ilikuwa na mishale inayong’aa na sauti iliyosikika kwa nguvu zaidi.
Alipoigusa ghafla sauti ilisikika “Mimi ni saa ya muda. Naweza kukusaidia… au kukuchelewesha milele.”Omari alishtuka. “Ina maana gani hiyo?”Saa ilijibu “ikisema baadaye nitakuonesha maana yake.”Omari hakuelewa sana lakini aliichukua saa ile na kuiweka chumbani kwake.
Siku iliyofuata bibi yake alimwambia aende sokoni kununua vitu. Omari alisema kama kawaida “Nitaenda baadaye.” Ghafla kila kitu kilibadilika!
Alijikuta bado yuko nyumbani lakini jua lilikuwa tayari limezama. Soko lilikuwa limefungwa na bibi yake alikuwa amekasirika.“Ilikuwa kazi rahisi tu!” bibi yake alisema kwa huzuni.
Omari alishangaa. “Lakini nilikuwa na muda…”
Saa ilisema kuwa “Muda ni zawadi ukicheza nao utakuchezea pia.”
Kuanzia siku hiyo Omari alibadilika. Kila alipopewa kazi aliifanya mara moja bila kusema “baadaye.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment