UPENDO NI MUHIMU KULIKO ZAWADI ZA GHARAMA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Juma alikuwa mvulana mdogo aliyeishi na mama yake katika nyumba ndogo. Mama yake alikuwa anafanya kazi ya kuuza mboga sokoni ili waweze kupata chakula na ada ya shule.

Siku moja Juma alisikia kuwa ilikuwa inakaribia Mother's Day. Watoto wenzake walikuwa wakizungumza kuhusu zawadi watakazonunua kwa mama zao.

Juma alihuzunika kidogo kwa sababu hakuwa na pesa ya kununua zawadi.

Alifikiria sana kisha akapata wazo. Baada ya shule alianza kusaidia kazi zote za nyumbani bila kulalamika kusafisha nyumba, kufua na hata kupika chakula kidogo alichoweza.

Pia alichukua karatasi ya zamani na kuandika ujumbe: “Asante mama kwa kunijali na kunipenda. Nakupenda sana nakuombe kwa Mungu uishi miaka mingi”.

Siku ya Mother's Day ilipofika alimkabidhi mama yake ule ujumbe.

Mama yake aliposoma machozi yalimtoka. Akamkumbatia Juma na kusema: “Hii ndiyo zawadi nzuri kuliko zote niliyowahi kupata.”

Juma alitabasamu na kujua kuwa hata bila pesa aliweza kumfurahisha mama yake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments