UBUNIFU HULETA MATOKEO MAZURI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na msichana aitwaye Lila. Lila alipenda sana kupiga picha na kutengeneza vitambulisho vidogo vya karatasi kwa ajili ya familia na marafiki zake.

Siku moja aliamua kujaribu kupiga picha nzuri za bustani ya shule kisha kuunda kadi ndogo za pongezi kwa kila mwanafunzi aliyepita karibu. Lakini wakati alipojaribu kuchapisha kadi zake rangi ziliingia kwenye karatasi nyingine na baadhi ya picha zikaharibika.

Lila alihisi kukata tamaa kwa muda mfupi. Lakini alikumbuka jambo alilojifunza: “Kila makosa ni nafasi ya kujifunza kitu kipya.”

Alipanga tena kadi akajaribu kutumia rangi kwa uangalifu zaidi na hata kuongeza vipengele vya ubunifu kama mabao madogo na michoro midogo.

Baada ya muda kadi zake zilikamilika kwa urembo mkubwa zaidi na kila mwanafunzi aliopokea alifurahia sana. Lila alijifunza kuwa kubadilisha makosa kuwa nafasi ya kujifunza huleta matokeo bora zaidi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments