Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kassim alikuwa mwanafunzi aliyekuwa anafanya vibaya sana darasani. Alikuwa hapendi kusoma na mara nyingi alikuwa akichelewa shule.
Walimu wengi walimchukulia kama mwanafunzi asiyejali.
Siku moja mwalimu mpya aliingia shuleni. Alikuwa anaitwa Mwalimu Daniel. Alipoanza kufundisha aligundua Kassim alikuwa kimya sana lakini macho yake yalionesha kama ana jambo ndani yake.
Baada ya kipindi alimuita na kumuuliza “Kwa nini hupendi kusoma?”
Kassim alinyamaza kwa muda kisha akasema kwa sauti ya chini “Nyumbani hakuna mtu wa kunisaidia… na wakati mwingine nakosa hata muda wa kusoma.”
Mwalimu Daniel alielewa. Badala ya kumkemea alianza kumpa muda wa ziada baada ya shule. Alimfundisha polepole na kumpa moyo.
Wiki zilipita Kassim alianza kubadilika. Alianza kuelewa masomo na hata kujiamini zaidi.
Wanafunzi wenzake walishangaa kuona mabadiliko yake.
Siku ya matokeo Kassim alipata alama nzuri kuliko hapo awali. Alimfuata mwalimu wake na kusema “Asante kwa kuniamini.”
Mwalimu Daniel alitabasamu na kusema “Kila mtoto anaweza akipewa nafasi.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment