Emakulata Msafiri
mwanakwetukids.
Mama yake alimwambia mara nyingi “Kelvin usisahau masomo yako.”
Lakini Kelvin alikuwa akijibu “Nitasoma baadaye hii game iko karibu kuisha!”
Siku moja shuleni mwalimu aliwatangazia wanafunzi kuwa kutakuwa na mashindano ya ubunifu wa teknolojia. Mshindi angepata zawadi kubwa na nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu kompyuta.
Rafiki yake Kelvin alisema “Hii ni nafasi nzuri tushiriki pamoja!”
Lakini Kelvin akasema “Mimi siwezi sina muda… lazima nicheze Free Fire.”
Asha akaamua kushiriki peke yake. Alijitahidi sana akatumia muda wake kujifunza na kutengeneza mradi mdogo wa app ya kusaidia wanafunzi kupanga ratiba zao.
Siku ya mashindano ilipofika Asha alishinda! Alipongezwa na walimu na wanafunzi wote.
Kelvin aliposikia alijisikia vibaya. Aligundua kuwa muda mwingi aliutumia kwenye game badala ya kujenga maisha yake.
Alimfuata Asha na kusema “Samahani nilikosa nafasi nzuri. Naomba unifundishe jinsi ya kuanza.”
Asha akatabasamu “Bado hujachelewa unaweza kubadilika.”
Kuanzia siku hiyo Kelvin alianza kupunguza muda wa kucheza na kuanza kujifunza mambo mapya. Bado alicheza game lakini kwa kiasi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment