KUWA HALISI NI BORA KULIKO KUIGIZA MAISHA

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijana aitwaye Musa aliyependa sana kutumia Facebook. Kila siku alikuwa anapost picha za maisha ya kifahari magari, chakula kizuri na sehemu za gharama kubwa ingawa nyingi hazikuwa zake.

Alikuwa anakopa vitu vya rafiki zake au kupiga picha sehemu ambazo si zake ili watu waamini ana maisha makubwa. Watu wengi walikuwa wanamfuata na kumpa likes nyingi.

Siku moja alikutana na kijana mwingine aitwaye Baraka aliyekuwa na maisha ya kawaida sana. Hakupost sana kwenye Facebook lakini kila alipost ilikuwa ni kuhusu kazi yake na juhudi zake.

Baraka alimwambia Musa “Maisha ya kweli hayahitaji kuigizwa. Ni bora kuwa wewe mwenyewe.”

Musa hakumjali sana mwanzoni. Lakini siku moja mmoja wa followers wake alitaka kukutana naye ili ajifunze jinsi ya kufanikiwa kama yeye. Musa alishindwa hata kueleza ukweli akaanza kuhisi aibu.

Usiku huo alifikiria sana. Aligundua kuwa alikuwa anaishi maisha ya uongo mtandaoni.

Siku iliyofuata Musa aliamua kubadilika. Alipost ukweli wake akawaeleza watu kuwa alikuwa anaigiza maisha na sasa anataka kuanza upya kwa juhudi za kweli.

Cha kushangaza watu wengi walimheshimu zaidi kwa kusema ukweli kuliko hata zile picha za kifahari.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments