KUULIZA SI UDHAIFU BALI NI NJIA YA KUJIFUNZA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Asubuhi moja yenye upepo mwanana Rashidi alisimama nje ya nyumba yao akitazama watoto wengine wakipita wakielekea shule. Alishika begi lake kwa nguvu lakini hakuanza kutembea mara moja.

Rashidi alikuwa na changamoto moja alikuwa anaogopa kuuliza maswali darasani. Kila aliposhindwa kuelewa somo alinyamaza kimya akihofia kuchekwa na wenzake.

Siku hiyo mwalimu wao alianza kufundisha somo jipya la hesabu. Rashidi alijitahidi kufuatilia lakini hakuelewa vizuri. Moyo wake ulianza kwenda mbio. Alitaka kuuliza lakini alikaa kimya kama kawaida.

Baada ya kipindi rafiki yake alimwambia “Kama hujaelewa si uulize? Hata mimi sikuwa nimeelewa mwanzoni.”

Maneno yale yalimfanya Rashidi afikirie sana. Siku iliyofuata alipokuwa darasani tena mwalimu alipouliza kama kuna yeyote mwenye swali Rashidi alinyanyua mkono taratibu.

Darasa lilinyamaza. Rashidi alihisi kama kila mtu anamwangalia lakini alikusanya ujasiri na kuuliza swali lake.

Mwalimu alitabasamu na kusema “Swali zuri sana Rashidi. Wengi walikuwa wanahitaji ufafanuzi huo.”Wanafunzi wengine waliinua mikono pia wakisema walikuwa hawajaelewa. Rashidi alishangaahakuwa peke yake!

Kuanzia siku hiyo Rashidi aliacha kuogopa. Alianza kuuliza maswali na hata kuwasaidia wengine walipoelewa kidogo.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments