HATA WATOTO WADOGO WANAPENDA MABADILIKO MAKUBWA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kundi la watoto wanne: Laila, Sam, Neema na Hassan. Walipenda sana kwenda porini karibu na kijiji chao wakichunguza mimea, wanyama wadogo na mito midogo.

Siku moja waliona sehemu ya msitu ilikuwa imechakaa na taka nyingi. Laila alisema “Hii haikubaliki! Wanyama hawa wanakosa makazi.”

Watoto walianza kupanga kila baada ya shule, wachukue glavu, mifuko ya plastiki na kusafisha sehemu hiyo ya msitu. Wakati wa wikendi pia walikuwa wanawaleta watoto wengine kutoka kijijini kujiunga nao.

Baada ya miezi michache msitu ulionekana kama mpya. Wanyama wadogo walirudi, na watoto walijivunia sana kazi yao. Hassan alisema “Tazama! Tunaweza kufanya tofauti kubwa hata kama tuko wadogo.”

Laila aliongeza “Ndiyo tuendelee kulinda mazingira yetu. Hii ni urithi kwa kizazi kijacho.”

Watoto waligundua kuwa ikiwa wote wanashirikiana hata changamoto kubwa inaweza kushughulikiwa.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments