Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na familia moja mama, baba, dada mkubwa na mtoto mdogo aitwaye Zuri. Kila Jumapili familia hiyo walipanga kupika pamoja chakula cha mchana. Lakini kila mara jambo dogo lingekuja na kuchekesha.
Siku hiyo Zuri alitaka kujaribu kupika pancakes yenye umbo la wanyama. Alijaribu kumfanya baba yake aone jinsi alivyo hodari lakini ghafla pancake moja ikaanguka kwenye kichwa cha baba! Baba akacheka sana mama akacheka na dada akacheka zaidi.
Halafu mama alijaribu kuchanganya mchanganyiko wa keki na akasababisha unga kupuliza kwenye jicho la Zuri. Wote walicheka sana na Zuri alisema “Hii ndiyo pancake bora ya kicheko!”
Baada ya muda walimaliza chakula chao huku kila mmoja akicheka na kufurahia jinsi walivyofanya kazi pamoja. Zuri alijifunza kuwa nyumbani hata makosa madogo yanaweza kuwa ya kufurahisha na furaha kubwa inakuja wakati wote wanashirikiana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment