BIDII NA UVUMILIVU HULETA MAFANIKIO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Halima alikuwa msichana aliyeishi kijijini pamoja na bibi yake. Maisha yao hayakuwa rahisi walitegemea kilimo kidogo cha mahindi ili kuishi.

Kila siku asubuhi Halima alikuwa anaamka mapema kwenda shambani kabla ya kwenda shule. Wakati mwingine alifika darasani akiwa amechoka sana.

Wanafunzi wengine walimcheka: “Unaonekana mchafu kila siku!”

Halima aliumia moyoni lakini hakukata tamaa. Alijua kuwa elimu ndiyo njia ya kubadilisha maisha yake.

Usiku hata bila umeme alikuwa anasoma kwa kutumia taa ya mafuta. Bibi yake alikuwa akimwambia “Endelea mwanangu siku moja utafanikiwa.”

Miaka ilipita kwa uvumilivu na bidii.

Siku ya matokeo ya mwisho ilipofika Halima alifaulu kwa alama za juu sana kijijini kwao!

Alipata nafasi ya kujiunga na shule nzuri zaidi mjini.

Siku ya kuondoka alimkumbatia bibi yake na kusema: “Asante kwa kuniamini.”

Bibi yake alitabasamu kwa furaha na machozi ya furaha yakimtoka.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments