ZAWADI YA MWISHO YA BIBI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Emmy alikuwa msichana mdogo aliyeishi kijijini na bibi yake. Wazazi wake walifanya kazi mjini hivyo aliishi na bibi aliyempenda sana.

Kila asubuhi Emmy alimsaidia bibi kuchota maji, kufagia uwanja na kulisha kuku. Wakati mwingine alihisi kuchoka hasa alipowaona watoto wengine wakicheza.

Siku moja Emmy alilalamika kidogo “Bibi mbona nafanya kazi nyingi sana?”

Bibi alitabasamu na kusema

“Kazi si adhabu mjukuu wangu. Kazi inakufundisha kuwa na nguvu na kuwajibika.”

Baada ya muda bibi aliugua na kushindwa kufanya kazi. Sasa Emmy ndiye aliyekuwa akifanya karibu kila kitu nyumbani. Ingawa ilikuwa ngumu hakukata tamaa.

Miezi michache baadaye wazazi wake walirudi kutoka mjini. Walishangaa kuona Emmy ameweza kusimamia nyumba vizuri sana. Walimpongeza kwa kuwa mtoto mwenye bidii na moyo wa kusaidia.

Bibi alipona na kumwambia Emmy “Hiyo ndiyo zawadi yangu kwako nimekufundisha kuwa mtu wa kujitegemea.”

Emmy alitabasamu akagundua kuwa yale aliyoyaona kama mzigo yalikuwa mafunzo ya maisha.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments