WATOTO WANAPASWA KUWAHESHIMU NA KUWASIKILIZA WAZAZI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Tito aliishi na mama yake katika nyumba ndogo kijijini. Kila siku mama yake alikuwa anafanya kazi nyingi ili familia ipate chakula na mahitaji mengineyo.

Siku moja Tito aliporudi kutoka shule alimkuta mama yake amechoka sana baada ya kufanya kazi za nyumbani na shambani na alikua amejilaza kwenye mkeka mdogo uliochoka sana.

Tito akafikiria kidogo kisha akasema “Mama ngoja nikusaidie kazi naona umechoka sana”

Tito akaanza kufagia uwanja, akachota maji, akapanga vyombo na akapika chakula. Mama yake alifurahi sana kuona mtoto wake anamsaidia.

Mama akamwambia “Asante sana Tito. Mtoto mwema husaidia wazazi wake.”

Tito akasema “Nafurahi kukusaidia mama na pia najifunza vitu vipya vitakavyo nisaidia hata nikiwa mkubwa zaidi”.

Kuanzia siku hiyo Tito alikuwa akimsaidia mama yake kila alipoweza.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments