WAKATI WA HUZUNI UPENDO UNAWEZA KUWA NGUVU YA KUENDELEA MBELE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids i

Kulikuwa na mtoto mdogo aliyeitwa Jabari aliyeishi kijijini karibu na shule yake. Rafiki yake wa karibu alikuwa kijana aitwaye Shomari. Wawili hao walikuwa wapenzi wa michezo na kugawa siri kila siku.

Siku moja Shomari hakuenda shule. Jabari alifikiri ni kuwa amechelewa tu. Lakini baada ya saa kadhaa walipokea habari mbaya. Shomari alikuwa amepata ajali mbaya na hakupata kuishi.

Jabari alilia sana alihisi dunia yake imevunjika. Hakutaka kucheka, kucheza wala kwenda shule. Kila kitu kilikuwa kimetoweka. Wazazi wake walijaribu kumfariji lakini hapana maneno yaliyoweza kupunguza maumivu ya moyo wake.

Siku kadhaa baadaye Jabari aliamua kwenda kwenye mto walipokuwa wakicheza mara nyingi. Aliketi chini ya mti na kuzungumza kimya akimwambia Shomari maneno yake ya mwisho. Alijua rafiki yake hakuwa tena lakini alihisi uwepo wake kwa kila kicheko alichokuwa amekiona na kila mchezo walioshinda pamoja.

Kwa polepole Jabari alianza kuandika hadithi ndogo za Shomari kumbukumbu ya rafiki yake wa karibu. Kila alipoandika moyo wake ulianza kupoa kidogo ingawa huzuni bado ilikua ndani yake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments