USIOGOPE KUOMBA MSAADA UNAPOKUA NA SHIDA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Juma alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita. Baada ya shule alimsaidia baba yake kazi ndogo ndogo kama kuosha bodaboda na kupanga vitu nyumbani. Ingawa maisha hayakuwa rahisi Juma alikuwa na ndoto ya kuwa daktari siku moja.

Siku moja baba yake aliugua ghafla na hakuweza kwenda kazini kwa wiki moja. Hali ya nyumbani ikawa ngumu zaidi. Juma aliona aibu kuwaambia walimu wake kwamba hakuwa amelipa mchango wa shule.

Mwalimu wake wa darasa aligundua kuwa Juma alikuwa kimya sana siku hizo. Alimuita pembeni na kumuuliza shida yake. Kwa machozi Juma alimweleza hali ya baba yake.

Mwalimu aliguswa sana. Aliwaeleza walimu wengine na kwa pamoja wakaamua kumchangia baba yake pesa ya matibabu. Pia waliwasaidia kulipa mchango wa shule kwa muda huo.

Baada ya wiki chache baba yake alipona na kurudi kazini. Alishukuru sana walimu wa shule kwa msaada wao. Juma alijifunza kuwa kuzungumza ukweli na kuomba msaada si udhaifu.

Miaka ilipita Juma alimaliza shule kwa ufaulu mzuri. Aliahidi moyoni mwake kuwa siku atakapofanikiwa atawasaidia watoto wengine wanaopitia hali kama yake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments