USICHUKUE KITU KISICHO CHAKO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na paka mmoja aliyeitwa Miu. Miu alikuwa paka mzuri lakini alikuwa na tabia ya ajabu sana alipenda viatu kuliko samaki.

Kila mara mama wa nyumba aliponunua viatu vipya Miu alikuwa wa kwanza kuvijaribu. Alikuwa anaingia ndani ya kiatu kama anavaa soksi.

Siku moja mtoto wa nyumba alirudi kutoka shule na kuacha viatu vyake mlangoni.

Miu aliona viatu hivyo vipya na kusema “Ah! Viatu vipya! Lazima nivijaribu!”

Akaingia ndani ya kiatu cha kulia. Kisha akaingia ndani ya kiatu cha kushoto. Baada ya muda alijaribu kutembea.


Miu alijikuta anatembea kama mtu anayecheza dansi ya ajabu miguu yake iliteleza akaanguka kwenye kikapu cha nguo!

Mtoto alipoingia ndani aliona viatu vinatembea peke yake. Akaogopa na kupiga kelele

“Ah! Viatu vyangu vina roho!”

Mama alikuja haraka na kuona Miu akijaribu kutoka kwenye kikapu huku mkia wake ukining’inia.

Wote walicheka sana.

Baada ya siku hiyo Miu alijifunza kwamba viatu ni vya watu si vya paka.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments