Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Zamani, kulikuwa na tumbili mmoja aliyependa sana ndizi. Kila siku alitamani kula ndizi nyingi kuliko wanyama wengine.
Siku moja, aliona shamba la ndizi lililojaa ndizi nzuri sana. Lakini shamba lile lilikuwa la sungura.
Badala ya kuomba, tumbili aliamua kuiba ndizi usiku. Akaenda kimya kimya, akachuma ndizi nyingi na kuzikimbiza msituni.
Lakini alipokuwa anakimbia alijikwaa na kuanguka! Ndizi zote zikatapakaa chini. Sungura alisikia kelele na akaja haraka.
Alipomwona tumbili alisema kwa huzuni “Kwa nini umeiba badala ya kuniomba?”
Tumbili aliona aibu sana. Akasema “Samahani nilikuwa na tamaa.”
Sungura akamwambia “Kama ungeomba ningekupa. Lakini wizi si mzuri.”
Tumbili alijifunza somo lake na kuahidi kutorudia tena. Tangu siku hiyo alianza kuomba badala ya kuiba.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment