TEMBO NA NDEGE MDOGO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Msitu wenye miti mirefu aliishi tembo mkubwa sana. Tembo huyu alikuwa na nguvu nyingi na alijivunia sana ukubwa wake.

Siku moja ndege mdogo alijenga kiota chake juu ya mti. Alikuwa akifanya kazi kwa bidii kila siku kukusanya vijiti na majani.

Tembo alipita karibu na ule mti akasema kwa sauti kubwa

“Kiota chako ni kidogo sana! Mimi nina nguvu naweza kuuangusha mti huu kwa sekunde chache!”

Ndege mdogo hakukasirika. Alisema “Kila mmoja ana uwezo wake. Mimi ninaweza kuruka juu sana angani wewe unaweza?”

Tembo alikaa kimya kidogo lakini bado alijiona bora.

Siku chache baadaye upepo mkali na mvua kubwa zilianza kunyesha. Miti ilianza kuanguka na maji yakaanza kujaa kila mahali.

Tembo alihangaika sana kwa sababu hakuweza kukimbia haraka kwenye sehemu salama. Lakini ndege mdogo aliruka juu angani na kwenda mahali salama.

Baada ya mvua kuisha ndege alimwona tembo akiwa amechoka na mwenye huzuni. Akamwambia. “Usijivunie sana. Kila mmoja ana kipaji chake.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872





0/Post a Comment/Comments