Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aitwaye Amina. Amina alipenda sana kuchunguza vitu na kuuliza maswali mengi kila kukicha.
Siku moja alipokuwa akisafisha chumba cha bibi yake aliona sanduku la zamani chini ya kitanda. Sanduku lile lilikuwa limefungwa na lilionekana la ajabu sana.
Amina akamwita bibi yake na kumuuliza “Bibi kuna nini ndani ya sanduku hili?”
Bibi akatabasamu na kusema
“Hilo ni sanduku la siri. Lakini linafunguliwa tu na mtoto mwenye subira na tabia njema.”
Amina alitamani sana kujua kilichomo ndani. Kwa siku kadhaa alianza kusaidia kazi za nyumbani bila kulalamikabakawa mtiifu na mwenye heshima zaidi.
Baada ya muda biibi yake alimpa ufunguo wa sanduku. Amina akafungua kwa furaha kubwa… lakini ndani kulikuwa na kioo tu!
Amina akashangaa “Bibi mbona hakuna kitu?”
Bibi akasema “Kioo hicho kinaonyesha siri ya kweli mtoto mwema na mwenye subira ndiye hazina kubwa kuliko zote.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment