Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mvulana mdogo aitwaye Daniel aliyeishi kijijini. Familia yake ilikuwa maskini lakini walijaribu kuishi kwa furaha. Daniel alipenda shule, kucheza na marafiki na kusaidia wazazi wake nyumbani.
Siku moja baada ya mvua kubwa nyumba yao iliharibiwa na mito kujaa. Vitu vyote vya Daniel vilipotea daftari lake, vitabu, nguo na hata mchezo wake wa mpira aliopenda sana. Daniel alihisi dunia yake imevunjika hakujua ataanza wapi.
Mama yake alimkumbatia kwa upole na kusema “Daniel ingawa kila kitu kimepotea bado tuna tumaini na familia yetu. Tutaendelea pamoja.”
Daniel alilia sana lakini polepole alianza kuelewa maneno ya mama yake. Aliamua kusaidia kuokoa kile kidogo kilichobaki, kusaidia wazazi wake kujenga nyumba mpya na kuanza tena shule bila hofu.
Ingawa moyo wake ulikuwa umejaa huzuni Daniel alijifunza kuwa hata wakati kila kitu kinapotea upendo na mshikamano wa familia unaweza kuleta matumaini mapya.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment