Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Rahma alikuwa mwanafunzi wa darasa la pili. Siku moja alipofika shuleni aligundua kuwa amesahau penseli nyumbani. Alianza kuwa na wasiwasi kwa sababu mwalimu alisema wanafunzi wote wataandika kazi.
Rafiki yake Neema aliona Rahma ana huzuni akamsogelea kwa ukaribu na akamuuliza
“Kuna nini Rahma?”
Rahma akajibu “Nimesahau penseli nyumbani. Sasa sitaweza kuandika kazi.”
Neema akatabasamu na kusema “Usijali nina penseli mbili ninaweza kutumia moja.”
Rahma alifurahi sana. Aliandika kazi yake vizuri hadi ikaisha. Baada ya shule alimshukuru Neema sana kwa msaada wake.
Tangu siku hiyo Rahma alijifunza kuandaa vitu vyake mapema usiku kabla ya kwenda shule na pia alijua umuhimu wa kuwa rafiki mwema kwa wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment