POLEPOLE LAKINI KWA UHAKIKA HUFIKA MBALI

 

Emakulata Msafiri

Zamani kulikuwa na kobe mmoja aliyekuwa mpole na mwenye subira sana. Aliishi karibu na mto na kila siku alikuwa akifanya kazi zake polepole bila kulalamika.

Siku moja mbweha mjanja alimwona kobe na kuanza kumcheka

“Wewe ni mwepesi sana? Hapana! Wewe ni wa polepole sana! Huwezi kufanikiwa maishani!”

Kobe alitabasamu tu na kusema “Kila mmoja ana njia yake. Mimi nitafika ninapotaka hata kama ni polepole.”

Mbweha akamwambia “Basi tushindane mbio hadi ule mti mkubwa pale!”

Wanyama wengine walikusanyika kutazama mashindano. Mbio zilipoanza mbweha alikimbia kwa kasi sana na kumuacha kobe nyuma kabisa.

Njiani mbweha alijiamini sana akasema “Huyu kobe hawezi kunipata!”

Akaamua kupumzika chini ya mti lakini akalala usingizi mzito.

Wakati huo kobe aliendelea kutembea polepole bila kusimama. Hatimaye akampita mbweha aliyelala na kufika mwisho wa mashindano.

Wanyama walishangilia sana! Mbweha alipoamka alikuta tayari kobe ameshinda.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments