NYANI WADOGO NA SUNGURA BAHARINI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na nyani wadogo wawili Kito na Lila waliokuwa wakicheza karibu na mto mkubwa. Kila siku walipenda kukimbia na kupanda miti karibu na maji.

Siku moja waliona sungura mmoja akijaribu kuvuka mto kwa kutumia kijiti kidogo. Sungura alijaribu mara kadhaa lakini kijiti kiligongana na mawe na kuanguka tena na tena.

Kito alisema “Lila tunapaswa kumsaidia! Hawezi kuvuka peke yake.”

Lila akakubali na wote walikusanya vichaka na matawi ili kumsaidia sungura kufanya daraja dogo la kuvuka mto.

Sungura alishangaa na kusema “Shukrani sana hamkuniwacha peke yangu. Sasa naweza kuvuka salama!”

Baada ya hapo nyani na sungura walicheza pamoja kando ya mto wakicheka na kufurahia. Wote walijifunza kuwa kushirikiana kunaleta matokeo bora kuliko kila mmoja kufanya peke yake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments