Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana aitwaye Amina aliyeishi katika kijiji kimoja karibu na Ziwa Victoria huko Mwanza. Baba yake alikuwa mvuvi na mama yake alikuwa anauza samaki sokoni.
Amina alikuwa anasoma darasa la saba. Alikuwa mwerevu lakini mara nyingi alichelewa kufika shuleni kwa sababu asubuhi alipaswa kumsaidia mama yake kupanga samaki kabla ya kwenda darasani.
Siku moja alichelewa sana na mwalimu akamkemea mbele ya wanafunzi wote. Amina alijisikia vibaya na karibu alie. Lakini hakujibu kwa hasira. Baada ya kipindi alimfuata mwalimu na kumweleza hali ya nyumbani kwa heshima.
Mwalimu alimsikiliza kwa makini. Aligundua kuwa Amina hakuwa mvivu bali alikuwa na majukumu mengi nyumbani. Tangu siku hiyo mwalimu alimruhusu Amina kufidia muda aliochelewa kwa kukaa maktaba wakati wa mapumziko.
Amina alijitahidi sana kusoma. Usiku alikuwa akisoma kwa taa ya chemli kwa . Licha ya changamoto hakukata tamaa.
Matokeo ya mtihani wa mwisho yalipotoka Amina alikuwa mwanafunzi wa kwanza darasani. Kijiji kizima kilijivunia mafanikio yake. Wazazi wake walifurahi sana na walimwambia “Bidii yako imeleta heshima kwa familia yetu.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment