MANENO YA WAZAZI NI TIBA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hassan alikuwa mtoto anayesoma darasa la pili. Siku moja asubuhi alitoka nyumbani kwenda shule bila kuangalia hali ya hewa. Anga lilikuwa linaonekana kuwa na mawingu mengi lakini Hassan hakujali sana.

Alipofika shuleni masomo yalianza kawaida. Baada ya muda mawingu meusi yalijikusanya angani na mvua kubwa ikaanza kunyesha.

Hassan alishtuka kidogo kwa sababu hakubeba mwavuli wake. Alikumbuka kwamba alikuwa ameacha mwavuli nyumbani juu ya kitanda chake.

Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu. Hassan alianza kufikiria kuhusu mama yake na jinsi atakavyorudi nyumbani.

Baada ya kama saa moja mvua ilipungua kidogo. Hassan alitoka polepole na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwa tahadhari.Njiani alikumbuka maneno ya baba yake kwamba

“Ni vizuri kuangalia hali ya hewa kabla ya kutoka na pia kubeba vitu muhimu.”

Alipofika nyumbani mama yake alimwuliza

“Leo mvua imekushika?”

Hassan akajibu “Ndio mama lakini nimejifunza kuwa ni vizuri kujiandaa kabla ya kutoka.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments