Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Amina alipenda kusoma hadithi za watoto kila jioni kabla ya kulala. Familia yake haikuwa na pesa za kununua vitabu vipya lakini Amina aliridhika kusoma kitabu chake kilichokuwa na kurasa zilizovunjika.
Siku moja kitabu chake kipendacho kilipotea. Alitafuta kila kona ya nyumba lakini hakukipata. Amina alihisi moyo wake umevunjika kwani kitabu hicho kilikuwa rafiki yake mkubwa kila hadithi kilimfundisha kitu kipya na kumfanya aendelee kuota ndoto.
Mama yake aliona huzuni ya Amina na alimkumbatia. “Amina labda kitabu kimepotea lakini hadithi zako bado ziko ndani ya moyo wako. Tumia akili na moyo wako kuunda ndoto zako.”
Hapo Amina alikamata kalamu na karatasi ndogo. Aliandika hadithi zake mwenyewe akirudia kile alichojifunza kutoka kitabu kilichopotea. Polepole tabasamu lake lilirudi kwani alijua kuwa ndoto na maarifa hayana mwisho huweza kuundwa tena bila kitu cha kufungwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment