JUMA NA SIRI YA KUFIKA SHULE KWA WAKATI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Juma alikuwa mwanafunzi mzuri lakini alikuwa na tabia ya kuchelewa shuleni. Kila asubuhi alikuwa anaamka mapema lakini alikua anajiandaa polepole sana.

Siku moja alipofika shuleni akiwa amechelewa mwalimu alimwambia

“Juma kuchelewa kunakufanya upoteze masomo muhimu na pia itapelekea hata ufeli masomo yako usipojirekebisha hiyo tabia yako.”

Juma alisikia aibu na akainamisha kichwa chini kana kwambwa anaona haya. Alipoenda nyumbani alimwambia mama yake kuhusu tatizo hilo la kuchelewashuleni.

Mama yake akamwambia “Jaribu kuamka mapema na ujitayarishe usiku vitu vyako vya shule kabla ya kulala.”

Kuanzia siku hiyo Juma alianza kuweka sare yake tayari usiku na akaanza kuamka mapema kuliko kawaida.

Baada ya muda hakuwahi kuchelewa tena shuleni. Mwalimu wake alimpongeza kwa kubadilika na kuwa mwanafunzi anayewahi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments