Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kuna mtoto aliyeitwa Baraka. Baraka alikuwa na rafiki yake aliyeitwa Kato. Mwanzoni Baraka alifikiri Kato alikuwa rafiki mzuri sana kwa sababu walicheza pamoja na kwenda shule pamoja.
Lakini Kato alikuwa na tabia ya ajabu. Alikuwa anacheka na Baraka akiwa mbele yake lakini akimsema vibaya nyuma yake kwa watoto wengine.
Siku moja Baraka alipoteza penseli yake shuleni. Alimwambia Kato
“Rafiki nimepoteza penseli yangu. Unaweza kunisaidia kuitafuta?”
Kato akasema “Ndiyo tutatafuta.”
Lakini baada ya Baraka kuondoka kidogo Kato aliwaambia watoto wengine
“Baraka ni mzembe sana hata penseli yake anaweza kupoteza.”
Baadaye mwalimu alileta penseli iliyopatikana darasani na akasema inaweza kuwa ya Baraka. Baraka alifurahi.
Siku nyingine Baraka alisikia watoto wakimsema vibaya kuhusu jambo ambalo alijua ni Kato alikuwa amewasemea.
Baraka alihuzunika sana lakini hakugombana na Kato. Badala yake Baraka alimwambia Kato,
“Rafiki wa kweli husema ukweli mbele na nyuma.”
Kato aliona aibu kidogo na kuanza kubadilika polepole. Akaacha kusema vibaya kuhusu Baraka.
Baada ya muda urafiki wao ukawa mzuri zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment