Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mvulana mdogo aitwaye Juma. Siku moja alipewa mwavuli na mama yake kabla ya kwenda shule. Mama yake aliona hali ya hewa ni kama ya mvua maana wingi lilikua jeusi angani.
Mama akamwambia “Usiupoteze huu mwavuli utakulinda wakati wa mvua itakapo anza kunyesha ili usilowane.”
Juma hakujali sana. Aliona jua linawaka akasema moyoni
“Leo hakuna mvua.”
Njiani alikutana na rafiki zake na kuanza kucheza. Kwa bahati mbaya aliusahaau mwavuli wake chini ya mt pindi anacheza.
Baada ya muda mawingu meusi yakakusanyika angani na mvua kubwa ikaanza kunyesha! Watoto wote wakaanza kukimbia kutafuta pa kujikinga. Juma akakumbuka mwavuli wake lakini ulikuwa mbali.
Alilowa kabisa na kufika shule akiwa na baridi na huzuni.
Aliporudi nyumbani mama yake akamuuliza mbona umelowa hivyo na mwavuli ulibeba?
Juma akajibu kwa kuona haya na kusema mwavuli nilisahau chini ya mti nilipokua na cheza na marafiki zangu.
Mama akasema “Umeona umuhimu wa kutunza vitu vyako?”
Juma akasema kwa aibu “Ndio mama sitarudia tena".
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872





Post a Comment