Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
“Mama leo nitasaidia shamba!” Imani alisema kwa shauku akipakia kikapu chake cha rangi ya bluu na kuanza kumfata mama yake nyuma polepole.
Lakini kumbukakazi lazima ufanye kwa makini mama yake alisema akitabasamu.
Imani alikwenda shambani akipanda mbegu, kumwagilia mimea na kuvuna baadhi ya mahindi yaliyokomaa. Alijua kazi ilikuwa ngumu lakini moyo wake ulikuwa mkali. Wakati wa mapumziko akaangalia shamba lote. Mimea ilikuwa inakua kidogo kidogo.
“Angalia hapa!” Imani akasema kwa furaha. “Mimea hii sasa inaisha kuota!”
Mama yake alimpongeza kwa uchapakazi wake alioonesha.
“Umefanya kazi nzuri Imani. Hii ni matokeo ya bidii yako ni muhimu kujituma kila siku.”
Siku ile Imani alijifunza kuwa hata mtoto mdogo anapojituma kazi ndogo ndogo inaweza kuleta matokeo makubwa. Alirudi nyumbani akiwa na furaha na moyo wa kuendelea kusaidia kila siku.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment