Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Heri alikuwa mvulana mdogo wa miaka 9 aliyeanza shule mpya karibu na shamba la familia yake. Shule yao ilipanga mradi maalum wa bustani kila mwanafunzi angepanda mimea na kujifunza jinsi ya kulinda mazingira.
Siku ya kwanza walimu waliwaeleza watoto
“Leo kila mmoja atapata kipande kidogo cha shamba. Kila mimea itapandwa kwa makini na tutajifunza jinsi ya kuilinda.”
Heri alipata kipande chake karibu na mto mdogo. Alijua kuwa kulima hakukuwa rahisi lakini moyo wake ulikuwa mkali. Aliweka mbegu, kumwagilia mimea na kuondoa majani yaliyoanguka. Wakati wa mapumziko alichunguza mimea yote akiona baadhi ikianza kuota polepole.
Wakati wa chakula cha mchana walimu waliwauliza
“Ni kitu gani mumejifunza leo?”
Heri alikumbuka jinsi alivyochangamka kutunza mimea na jinsi alivyoshirikiana na wenzake
“Nilijifunza kuwa kwa bidii na kushirikiana na marafiki mimea yetu inaweza kukua vizuri.”
Mwisho wa siku Heri alirudi nyumbani akiwa na furaha. Alimwambia mama yake yote aliyojifunza.Kazi ngumu, kushirikiana na kujituma huleta matokeo mazuri.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment