EmakulataMsafiri
Mwanakwetukids
Faraja alikuwa mtoto mdogo aliyeishi kijijini. Siku moja mama yake alimpa pesa kidogo na kumuagiza aende sokoni kununua mboga na matunda kwa ajili ya familia.
Akiwa sokoni Faraja aliona mtoto mdogo akilia kwa sababu hakukuwa na pesa ya kununua chakula. Faraja alifikiria kwa sekunde chache kisha akamwambia:
“Chukua kipande hiki cha tunda mimi nitapata kingine nyumbani.”
Ingawa Faraja hakuzingatia kwamba matunda ameagizwa nyumbani alichotazama yeye ni upendo kwa yule mtoto aliyekua na shida ya chakula wakati ule.
Mtoto huyo alifurahi sana na kumshukuru Faraja. Faraja alirudi nyumbani akiwa na furaha akijua kuwa kusaidia wengine ni jambo zuri zaidi kuliko kula matunda yote peke yake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment