ASHA NA SHULE SIKU YA KWANZA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Asha alikuwa msichana wa miaka 7 aliyeanza shule kwa mara ya kwanza. Alikuwa na hofu kidogo kwa sababu hakuwahi kuondoka nyumbani bila mama yake. Siku ya kwanza shuleni aliingia darasani akiwa na kitabu chake kipya na begi lake.

Walimu walimkaribisha na kumtambulisha kwa wenzake. Wengine walicheka na kucheza kwa urahisi lakini Asha alikuwa kimya na kuogopa kuzungumza. Alijaribu kukaa kando akitazama kila jambo kwa makini.

Wakati wa mapumziko watoto wengine walianza kucheka kwa pamoja. Asha alihisi pweke lakini alikumbuka maneno ya mama yake.

“Usiogope kujaribu Asha. Jaribu kuzungumza na wenzako.”

Asha akaamua kuanza kidogo. Alimwambia mtoto mmoja aliyeketi karibu

“Unacheza mchezo gani?”

Mtoto huyo akatabasamu na kusema “Unataka kujiunga nami?”

Asha akakubali na walicheza pamoja. Polepole akaanza kuzungumza na watoto wengine. Siku hiyo alirudi nyumbani akiwa na furaha na hadithi za kuchekesha za watoto wake wenzake.

Mama yake akamuuliza “Leo shuleni uliwahi kucheka na wenzako?”

Asha alitabasamu na kusema “Ndio mama nilijua ni vigumu mwanzoni lakini sasa ni furaha!”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments