ASHA NA MFUKO WA SHULE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Asha alikuwa msichana mdogo aliyeishi na mama yake katika kijiji kidogo. Kila siku alikuwa anaenda shule kwa miguu akiwa na mfuko wake wa vitabu mgongoni.

Siku moja alipokuwa anarudi kutoka shule Asha aliona mfuko mdogo wa pesa njiani. Aliuchukua na kuufungua. Ndani kulikuwa na pesa nyingi.

Asha alishangaa sana. Akasema “Hizi pesa si zangu. Lazima nimtafute mwenyewe.”

Aliendelea kutembea mpaka akafika dukani kwa mama mmoja aliyekuwa analia. Asha akamuuliza “Mama kwa nini unalia?”

Mama yule akasema “Nimepoteza mfuko wangu wa pesa. Nilikuwa naenda kununua dawa za mtoto wangu.” Asha akatoa ule mfuko na kusema

“Je huu ndio mfuko wako?” Mama yule alifurahi sana akasema

“Ndio! Huu ndio mfuko wangu.”



Mama alimshukuru sana Asha kwa uaminifu wake. Baadaye alimwambia mwalimu wa shule kuhusu kitendo cha Asha. Siku iliyofuata Asha alisifiwa mbele ya wanafunzi wote kwa kuwa mwaminifu na mwenye moyo mwema.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments