AISHA NA KIKOMBE CHENYE MAJI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Aisha alikuwa mtoto mdogo aliyeishi na familia yake kijijini. Kila siku kabla ya kwenda shule alikuwa akichukua kikombe cha maji kutoka kisima ili familia yake iwe na maji ya kunywa.

Siku moja kikombe chake kilikuwa kilipasuka kidogo na maji yalimwagika barabarani. Aisha alihisi huzuni sana kwa sababu hakuweza kupeleka maji yote nyumbani.

Njiani Aisha alipokua anarudi nyumbani alikua na maswali mengi akijiuliza. "Sasa Nitafanyaje kikombe changu kimepasuka na wapi nitapata kikombe kama hiki au nimwambie mama aninunulie kama hiki lakini hela mama atapata wapi nyingine na maisha magumu kwetu". Aisha alisema.

Mama yake alimuona Aisha akija kwa mbali lakini sura yake ilikua hiana matumaini kabisa alipofika nyumbani Aisha akamuuelezea mama yake kuhusu kikombe chake.

Mama akasema "usijali Aisha umejaribu na hiyo ndiyo muhimu nikipata hela nitakununulia kama hiki".


Aisha alijifunza kuwa kujaribu ni muhimu kuliko matokeo na kuwa makini zaidi kwenye siku zinazofuata.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments