AHADI YA MWISHO YA BIBI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Asha. Asha aliishi na bibi yake katika kijiji kidogo baada ya wazazi wake kufariki. Bibi yake alikuwa mzee sana lakini alimpenda Asha kwa moyo wote.

Kila siku Asha aliamka mapema na kusaidia kazi za nyumbani kisha huenda shule. Licha ya maisha kuwa magumu Asha alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa na mtu wa kumjali bibi yake.

Siku moja bibi yake alianza kuumwa. Asha alijaribu kumhudumia kadiri alivyoweza lakini hali ya bibi yake ilizidi kuwa mbaya. Hakukuwa na pesa za kutosha za kumpeleka hospitali.

Usiku mmoja Asha alikaa karibu na bibi yake akimshika mkono. Bibi yake alimwangalia na kusema kwa sauti ya upole, “Asha uwe na moyo wa nguvu. Soma kwa bidii maisha yako yatabadilika.”

Asubuhi ilipofika bibi yake alikuwa amefariki.

Asha alilia sana. Alijisikia mpweke na mwenye huzuni kubwa. Lakini alikumbuka maneno ya mwisho ya bibi yake. Alijifuta machozi na kuamua kuendelea kusoma kwa bidii, hata kama moyo wake ulikuwa umevunjika.

Miaka ilipita Asha alimaliza shule na kupata kazi nzuri. Ingawa bado alimkumbuka bibi yake kwa huzuni alijua kuwa angefurahi kumuona akifanikiwa.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments