UMUHIMU WA MAJI KWA WATOTO

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Maji ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. Hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuishi bila maji. Watoto kama binadamu wengine wanahitaji maji kila siku ili kuwa na afya njema na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Maji husaidia mwili wa mtoto kufanya kazi vizuri. Mtoto anapokunywa maji ya kutosha mwili wake huweza kusafirisha chakula kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kutoa taka mwilini kupitia mkojo na jasho. Hii husaidia mwili kubaki safi na wenye nguvu.

Pia maji husaidia kuzuia magonjwa. Kunywa maji safi na salama huzuia magonjwa kama kuhara kipindupindu na homa ya matumbo. Pia maji hutumika kunawa mikono kuoga na kusafisha mazingira hivyo kusaidia kuondoa vijidudu vinavyosababisha magonjwa.

Aidha maji husaidia watoto kukua na kusoma vizuri. Mtoto anayekunywa maji ya kutosha huwa na nguvu ya kucheza kusoma na kushiriki vizuri darasani. Ukosefu wa maji unaweza kumfanya mtoto achoke haraka na ashindwe kuzingatia masomo.

Kwa ujumla maji ni uhai na ni muhimu sana kwa watoto. Ni wajibu wa wazazi walimu na watoto wenyewe kuhakikisha wanatumia na kunywa maji safi na salama kila siku ili kuishi maisha yenye afya na furaha.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments