SUNGURA NA MTI WA MAAJABU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hapo zamani za kale kulikuwa na sungura mdogo aliyeitwa Kiki. Kiki alipenda sana kucheza kuliko kusikiliza wazazi wake. Kila siku alikimbia porini kucheza na marafiki zake.

Siku moja Kiki aliona mti mkubwa wenye matunda ya rangi ya dhahabu. Alifurahi sana na kukimbia kuyachuma. Lakini kabla hajayachukua kobe mzee alimwambia

“Kiki usichukue matunda hayo bila ruhusa. Mti huu una sheria zake.”

Kiki hakusikiliza. Alikula tunda moja ghafla akaanza kupiga chafya bila kuacha!


“Achuuu! Achuuu!”

Aliogopa sana akamkimbilia kobe yule. Kobe akamwambia

“Mti huu unawapa zawadi wanaosikiliza lakini unaadhibu wasiotii.”

Kiki akaomba msamaha kwa sauti ndogo. Mara moja chafya ikaisha. Kuanzia siku hiyo Kiki akawa sungura msikivu na mwenye adabu.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments