Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Rehema alikuwa mtoto wa darasa la tano. Kila asubuhi alitembea umbali mrefu kwenda shule. Viatu vyake vilikuwa vimechakaa lakini hakuwahi kulalamika.
Siku moja shuleni watoto wenzake wakaanza kumcheka kwa sababu ya viatu vyake. Rehema alihisi uchungu moyoni lakini hakujibu chochote. Aliendelea kusoma kwa bidii.
Jioni alipofika nyumbani alimsaidia mama yake kuuza mboga sokoni. Mama alimwambia
“Rehema subira na bidii zako zinaonekana.”
Baada ya miezi michache Rehema alifanya vizuri sana kwenye mitihani. Shule ilimchagua apatiwe msaada wa vifaa vya shule. Miongoni mwa vitu hivyo kulikuwa na viatu vipya.
Rehema alivaa viatu vile kwa furaha lakini hakuwadharau waliomcheka awali. Aliendelea kuwa mnyenyekevu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment