Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Doris alikuwa msichana wa miaka kumi aliyeishi kijijini pamoja na wazazi wake. Kila asubuhi kabla ya kwenda shule alikuwa na jukumu la kuchota maji mtoni na kuwasaidia wazazi wake kulisha kuku.
Wakati mwingine Doris alichelewa shule kwa sababu ya kazi hizo. Lakini hakulalamika alijua kusaidia familia ni muhimu.
Siku moja mwalimu aliwaambia wanafunzi waandike insha kuhusu uwajibikaji. Doris akaandika kuhusu maisha yake ya kila siku nyumbani na jinsi anavyosaidia familia yake.
Mwalimu aliposoma insha ya Doris aliguswa sana. Akasema
“Huyu ni mtoto mwenye kuwajibika na mwenye moyo wa kusaidia wazazi nyumbani na pia nawaomba wanafunzi muige mfano huu wa Doris”.
Doris alipata zawadi ndogo ya kalamu na daftari. Alijisikia fahari sana na akaendelea kuwa mtoto mtiifu na mwenye bidii shuleni na nyumbani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment